Social Icons

Pages

Alhamisi, 21 Mei 2015

MJUE PRODUCER MTANZANIA AITWAYE FRAGA ALIYETENGENEZA NGOMA YA WASANII WAWILI WAKUBWA KUTOKA NCHINI NIGERIA.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi. 

WASIFU:-

Frank Mjack almaarufu kwa jina la Fraga au Mdogo wake Jaymillions ni Mhaya (amezaliwa tarehe 12 Novemba miaka kadhaa iliyopita, Wilayani Bukoaba Mkoani Kagera nchini Tanzania bara la Afrika), ni mtayarishaji wa muziki katika Studio za “Uprise Music Empire” na mwanamuziki wa muziki aina ya RnB, Afro Pop na Zuku. Ana elimu ya Kidato cha nne na baadae alifanikiwa kuingia Chuoni kusomea masuala ya muziki(Sound Engineering).

Hivi karibuni dhahiri shairi muziki unadaiwa kuwa ni moja ya tiba kwa wagonjwa baada ya watafiti kadhaa wa Chuo Kikuu cha Lomalinda nchini Marekani kuwaweka wagonjwa 100 katika chumba chenye muziki na wengine 100 kupelekwa hospitalini lakini waliowekwa katika chumba maalumu chenye muziki walioneka kupona mapema, kwa mantiki hii kazi zilizotayarishwa na “Fraga” zaweza kuwa ni dozi tosha.

“Fraga” amefanikiwa kufanya kazi na Wasanii wa nchini Nigeria kwa kutayarisha/kutengeneza remix ya wimbo uitao “Oga Thomas” wa mwana dada “Papa” aliomshirikisha msanii na mtayarishaji wa muziki mkubwa nchini Nigeria aitwaye “Selebobo”.

 Huu ni wimbo  wenyewe:-
Unaweza ukawa unajiuliza ni wapi Mtayarishaji huyu wa Kitanzania “Fraga” alikutana wapi na wasanii hawa wa Kinigeria? “Papa na Selebobo hawa ni wasanii wakubwa nchini Nigeria, huyu dada “Papa” ambaye ndio mwenye huu wimbo tulikutana kupitia Instagram mpaka ikafikia wakati akaniamini nakunipa kazi ya kufanya remix ya nyimbo yake”.
Hii ni video yake Papa.

Ilikujua kiundani zaidi sikuishia hapo niliendelea kudadisi zaidi kwa kupanua mahojiano baina yangu na “Fraga” ili kujua anaionaje taswira ya mbele katika zake. Na hii ni sehemu ya mahojiano yetu:-
CHRIS BEE :- Unadhani kufanya kazi na msanii PAPA itakuwa na faida gani kwako?
FRAGA:- Unajua kwanza ni hatua kubwa, kufanya kazi na kazi yako ikaaminiwa pia ni hatua ambayo nimepiga kufanya kazi International Artists wamesikiliza, watasikiliza wengi hivyo itanipatia wigo wa kufanya kazi nyingi international coz ata producer Selebobo ndiye aliye produce original version ya “Oga Thomas” amekubali sana uwezi amini nae anataka nimtengenezee mdundo arecord hii ni hatua muhimu kwangu muziki wangu unakua na kuaminiwa Afrika na DunianI kwa sasa ikaheshimiwa.

CHRIS BEE :- Okay, je kuna makubaliano yoyote ya kudumu yanayowafanya kuendelea kufanya kazi zaidi na Papa?
FRAGA:- Yeah baada ya hii kazi pia kuna beat yangu ambayo nimempatia, ataandika mistari yake na kurecod sauti huko kwao then atanitumia data ya vocal nitafanya mixing then namtumia ngoma yake ambayo ataiachia kwao, pia hii niliyomfanyia kwao itatoka kama remix ambayo beat kutoka kwa producer Fraga kutoka nchini Tanzania Tanzania.

CHRIS BEE :- Ni producer gani anakuvutia?
FRAGA:- Duniani nampenda sana "Timberland" ndiye producer ambaye nilikua nasikiliza kazi zake wakati najifunza uproducer.

CHRIS BEE :- Ni mambo gani yanayokutambulisha kama Fraga?
FRAGA:- Kwanza ni sign ninayotumia kwa kila wimbo ninao produce ambayo ni "Eyoooh Fraga” pia mtindo wangu wa kuproduce muziki Mungu kanijaalia sikio nzuri lakuweza kufanya muziki mzuri na msafi hivyo kwa mtu ambaye amewahi kusikia kazi zangu lazima atajua na yule ambaye ajawahi kusikia akisikia mara moja anatamani kusikia zaidi.

 Producer Fraga akiwa na Mfalme wa Miduara Tanzania AT

CHRIS BEE :- Ulikutana vipi na Msanii na Mfalme wa miduara Tanzania AT?
FRAGA:- AT ni msanii mmoja wapo niliyekua na ndoto ya kufanya nae kazi hivyo mwaka jana nilimtafuta kwa lengo la kumshirikisha katika nyimbo yangu ambayo tulifanikiwa kufanya wimbo uitwao "Nitakuimbia" baada ya hapo aliridhishwa na utendaji kazi wangu na kutaka niendeleee kumfanyia kazi....  Ambapo nikamfanyia kazi yake mpya kwa sasa inaitwa "Sijazoea" na pia kuna kazi nyingi za kwake ambazo zitafuata baada ya hiyo zote nime produce mwenyewe.

CHRIS BEE :- Mbali na AT ni wasanii gani wakubwa umefanya nao kazi?
FRAGA:- Kuna Spince Seseme, Ally Nipashe, Flora Mvungi, Black Rhyno na wengine wengi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa na Msanii H Mama wakati wa matengenezo ya Ngoma ya Mkazurure.

CHRIS BEE :- Ni msanii gani mwingine Tanzania unafikiri ukifanya naye kazi unaweza kumfanya akaonekana wa kitofauti kuliko msanii yeyote?
FRAGA:- Kipindi naanza muziki macho yangu nilikua nimeyatoa kwa Banana Zoro huyu ndiye amanishawishi mimi niwe msaniii.... hivyo siku nikimfanyia kazi ndoto yangu itakua imekamilika na pia naamini nitamfanyia kitu kikubwa.

CHRIS BEE :- Kwa idadi ya haraka umetengeneza ngoma ngapi?
FRAGA:- Ni kama nyimbo 10 hivi hizo nazungumzia ngoma ambazo ziko kwenye media na zinapata airtime ila ni nyingi sana ambazo nime produce za wasanii azijapata nafasi tu ila ni nzuri na nafikiri sababu inayochangia ni kutokana na wasanii kukosa menejimenti au connection au pesa za kufanyia promotion.

CHRIS BEE :- Una mpango wowote wa kusomea zaidi muziki?
FRAGA:- Elimu yangu ya Muziki bado sana nina mipango ya kujiendeleza kimasoma, pia mwaka jana mwezi wa kwanza niliingia chuo nikasomea Sound engineer lakin bado nahitaji elimu zaidi. Elimu aina mwisho kila nitakapo kua napata nafasi naingia darasani naongeza ujuzi.

 Fraga akitoa burudani katika moja ya Tamasha nchini Tanzania.

CHRIS BEE :- Unauzungumziaje muziki wa Tanzania kwa sasa.

FRAGA:- Kiukweli muziki wa Tanzania unakua sana yaani ukizungumzia nchi zenye ushindani kimuziki uwezi sahau Tanzania, pia nitoe wito kwa madj na mapresenter wa Tanzania waupe nafasi muziki wetu ili Wanigeria na Wasouth wacopy muziki wetu kama baadhi ya wasanii Watanzania wanavyo wakopi waooo, muziki wetu ni mzuri sana ila bado haujapata nafasi ya kutosha.

Msomaji naamini utakuwa umeyafahamu mambo mengi yanayomhusu Mtayarishaji na Mwanamuziki Fraga, tumpe baraka ya kila la kheri ili kuipeperusha vema bendera ya Taifa la Tanzania katika tasnia ya Muziki nchini.

 Moja ya Cover ya ngoma aliiachia mwanzoni mwa mwaka 2015 iitwayo DUNIA NZIMA

NB;- Unaweza M-FOLLOW  pia FRAGA kupitia Instagram @producerfraga na Facebook kwa jina la FRAGA DE PRO. 
Imeandikwa na Chris Bee.

PICHA ZA MWANAMUZIKI NA MTAYARISHAJI WA MUZIKI NCHINI TANZANIA AITWAYE FRAGA KUTOKA STUDIO ZA UPRISE MUSIC.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi na Msanii My Self wakati wa kushoot video ya ngoma ya Struggling..

  Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa na Mmiliki wa studio hizo ambaye pia ni Mtayarishaji wa Muziki wa Kizazi kipya aitwaye Dupy.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa na Msanii H Mama wakati wa matengenezo ya Ngoma ya Mkazurure.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga akiwa amepozi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya H Mama.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga akiwa mizungukoni kitaani..

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga akiwa ndani ya studio za Uprise Music Empire.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Moja ya Cover ya ngoma aliiachia mwanzoni mwa mwaka 2015 iitwayo DUNIA NZIMA

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga akiwa ndani ya studio za Uprise Music Empire.

 Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

 Fraga akitoa burudani katika moja ya Tamasha nchini Tanzania.

 Fraga akitoa burudani katika moja ya Tamasha nchini Tanzania.

 Producer Fraga akiwa na Mfalme wa Miduara Tanzania AT

Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki Tanzania aitwaye Fraga kutoka studio za Uprise Music Empire akiwa katika pozi.

WATCH:- FRAGA - KUPATIA{Official HD Music Video}

Blogger Templates